TAARIFA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) KUHUSU MFUMO MPYA WA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO

74 Comments
2110 Views

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) anapenda kuyajulisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Umma kwa ujumla kuwa ulipaji wa ada mbalimbali za NGOs umeanza kufanyika kupitia Mfumo wa Malipo ya Serikali wa Kimtandao (Government Electronic Payment Gateway).

Utaratibu huu mpya wa malipo unapatikana kupitia Tovuti ya Wizara na Idara ya Uratibu wa NGOs (www.mcdgc.go.tz na tnnc.go.tz).
Katika tovuti husika, ingia kwenye eneo lililoandikwa ‘ NGOs MIS’ ili upate taarifa na maelekezo kwa ajili ya kupata Namba ya Malipo (Control Number).

Kwa maelezo zaidi piga simu namba + 225 737 569 584/ 255 737569583 au + 255 262963346

Kupakua nakala ya barua bonyeza chini hapa:
http://www.tenmet.org/wp-content/uploads/2019/03/NGO_tangazo-1.pdf


Tamko Dhidi ya Udhalilishaji wa Watoto

Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) ni mtandao unaoundwa na mashirika...

Enroute to GAWE 2019 #TukutaneHandeni #Elimu BoraHakiYangu

TEN/MET Secretariat hosted a Press Conference on the 2nd of...